• HABARI MPYA

    Friday, October 18, 2013

    WENGER AFIKIRIA 'KUMPIGA MKEKA' OZIL KESHO NA NORWICH

    KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger atafikiria kumpumzisha kiungo wake Mesut Ozil katika mchezo wa kesho dhidi ya Norwich.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ujerumani amepona licha ya kuumia goti akiichezea timu yake ya taifa dhidi ya Ujerumani Jumajnne usiku.
    Lakini huku klabu yake ikikabiliwa na mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund Jumanne, Wenger anaona bora kumpa mapumziko mchezaji huyo aliyemnunua kwa Pauni Milioni 42.
    Kifaa: Mesut Ozil aliumia akiichezea Ujeurmani ikishinda 5-3 dhidi ya Sweden
    He'll be right: Ozil was substituted late in the match but Arsene Wenger says he will play Norwich on Saturday
    Atakuwa fiti: Ozil alitolewa mwishoni katika mechi hiyo, lakini Arsene Wenger atacheza Norwich kesho
    Bacary Sagna na Santi Cazorla wote wanaweza kucheza dhidi ya Norwich baada ya kupona maumivu yao.
    Beki Sagna alikosa mechi ya sare ya 1-1 na West Bromwich Albion Oktoba 6 kutokana na maumivu ya nyama, wakati Cazorla amekuwa nje kwa wiki sita kutokana na matatizo ya kifundo cha mguu.
    Pamoja na hayo, Theo Walcott ataendelea kuwa nje kwa wiki mbili akiendelea kupata ahueni ya maumivu yake.
    Big return: Santi Cazorla could return for the first time since Arsenal's defeat of Tottenham in September
    Urejeo mzito: Santi Cazorla atarejea kwa mara ya kwanza kikosini Arsenal tangu Septemba
    Contender: Defender Bacary Sagna has also recovered from a hamstring injury and could be back for Arsenal
    Mshindani: Beki Bacary Sagna pia amepona na anarejea kikosini Arsenal
    Wakati huo huo, Wenger jana amesema kwamba Arsenal itaendelea na desturi yake ya kuinua vipaji vya makinda licha ya kuvunja rekodi yake ya usajili kwa kumnunua Ozil.
    Wenger alisema: "Naamini kwamba bado tunatakiwa kujishawishi mustakabali wa klabu hii upo katika kazi tunayoifanya ndani — kuendeleza wachezaji wetu, kusaka vipaji kwa hakika, itakapohitajika, tutauza wengi nje na kununua mchezaji,".
    Mshambuliaji Yaya Sanogo (mgongo) na Lukas Podolski (nyama) pia wanaendelea na matibabu, pamoja na kiungo Alex Oxlade-Chamberlain na Abou Diaby (wote goti).
    walcott
    podolski

    Abou Diaby
     Alex Oxlade-Chamberlain
    Maumivu: Wachezaji majeruhi wa Arsenal Theo Walcott (juu kushoto), Lukas Podolski (kulia), Abou Diaby (chini kushoto) na Alex Oxlade-Chamberlain (kulia)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WENGER AFIKIRIA 'KUMPIGA MKEKA' OZIL KESHO NA NORWICH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top